AND SAFARIS.
Kampuni hii ambayo sasa
inakuja kwa kasi kubwa, inampango
wa kuhakikisha mkoa wetu wa Kagera
unaungana na mikoa mingine nchini kote katika mchakato wa
kukuza secta ya utalii wa
ndani na nje,zoezi hili litaenda
sambamba na utangazaji wa
vivutio vyote vilivyomo
ndani ya vijiji
vyetu, kata zetu, wilaya zetu ,mkoa
wetu, nchi yetu pamoja vivutio vingine vya utalii
ulimwenguni kote.
Ukweli utabakia
kuwa mkoa wetu unao
vivutio vyenye kuwezesha
uwepo wa utalii katika sehemu mbalimbali ndani
ya mazingira tunayoishi.Wilaya ya
karagwe ambayo mwonekano wake
unakuwa ni wakushangaza na wa kuvutia kwa
kuwa na mabonde,miinuko,tambarare,mito ,ziwa,chemichemi ya maji
moto,madini ya bati,sehemu zilizohifadhiwa kwa
ajili wanyama pamoja
na makumbusho ya
kiongozi mashuhuri aliyekuwa
mzungumzaji wa Kiswahili
fasaha kabla ya Kiswahili kuwa
lugha ya taifa.
Wilaya ya karagwe
ina historia ya
kuwa kubwa kwani
mwanzoni iliweza kugawanywa
katika majimbo mawili
ya uchaguzi yani jimbo la
uchaguzi la karagwe na kyerwa.Wilaya hii imegawanyika
na jimbo la kyerwa na
kuitngeneza historia ya
wilaya ya karagwe
kuendelea kutukuka kwa kulitangaza jimbo
la uchaguzi la Kyerwa kuwa
wilaya mpya.Wilaya mpya ya
kyerwa tayari imeanza
kuendesha shughuli zake kama wilaya mpya.
Wilaya hii mpya
iko chini ya uongozi wa mh.Luth.Kanari Benedict Kitenga ambaye
ndiye mkuu wa wilaya hii mpya
kuanzia may 2012.Pamoja na hayo
ni vema tukaonesha nia ya
dhati kwa kuonesha mshikamano na ushirikiano kaika kuhakikisha tunaikuza
kimaendeleo wilaya yetu
mpya .wilaya hii mpya ambayo
wakazi wake ni wanyambo
asilia ifikie hatua
tuamini kuwa maendeleo
yake yatakua kwa kasi
kubwa sana hii
inadhihilishwa na mali asili
zilizoko ndani yake.Amini
usiamini wilaya hii inasehemu
kubwa ya eneo ambalo
liko katika angalizo la
kuwa hifadhi ya taifa
lijulikanalo kama pori la
akiba la mulongo
ikumbukwe kuwa pori hili lina
wanyama aina tofautitofauti isipokuwa
simba na twiga lakini pia
kundi la wanyama wakubwa watano lijulikanolo kama big five
duniani pia lipo
,ukiachana na hayo kipo
kivutio kinachotoa maji moto
au hot water
sping katika sehemu ya Mutagata kwenye kata
ya kamuli, pamoja na
kivutio hiki ni moja
ya vivutio adimu lakini
hakina maboresho yoyote yanayoweza
kukiingiza katika soko la
utalii.Madini ya bati au
tini mikoa iliyoendelea sehemu
ya madini ni
muhimu kwani hutoa
uwekezaji,nafasi ya ajira
na huwa ni
kivutio cha utalii .Madini
ya namna hii
ni neema katika nchi na
sehemu husika.
Kilimo cha mikono wakulima
wa wilaya hii huendesha shughuli za
kilimo kwa kutumia
mikono yao wenyewe
hiki ni kivutio cha utalii cha
kutosha kwani sehemu kubwa ya nchii
yetu huendesha kilimo
kwa trecta na ng’ombe
lakini pia sehemu
zote duniani watu
hawalimi kwa mikono.
Kilimo cha kahawa
hili ni zao
la kibiashara ambalo linalimwa na
nchi chache ulimwenguni
sisi Tanzania ni wazalishaji wadogo duniani pamoja na
hayo kahawa tanza nia
hulimwa katika mikoa
ya Kilimanjaro na Kagera
na wilaya ya karagwe
huzalisha kahawa nyingi
kuliko wilaya za za mkoa
wetu ,wenzetu pia wanapenda kufanya
utalii wa kuona
jinsi kahawa zinavyolimwa
kukua kwake mpaka uvunaji wake .wengine
hupenda kuona rangi
mti wa mkahawa
ambao mara nyingi huonekana
ukiwa wa kijani
mara nyingi.
Ufugaji, mpaka leo
wilaya hii mpya
ina wafugaji wengi
wa ng’ombe wa nyama
sehemu kubwa ya
siina .Hii ni
sehemu kubwa na inategemewa kwa
uzalishaji wa maziwa
,mfumo wa ufugaji
kwa jinsi gani
unaendeshwa kienyeji tunapenda
dunia ijue huu ni
utalii .
Uvuvi,nayo ni ni
moja ya
shughuli zenye uwezo
wa kuyageuza maisha ya
wakazi wa kyerwa. Lakini kwa sababu
wavuvi hawa wanatumia
mitumbwi ya kuchonga
bado hiki ni
kivutio cha utalii kwa
leo mitumbwi inayotumika katika
maziwa ya sehemu
nyingine ni ya
kisasa maboti na
fibire
Rangi ya kijani,
sehemu kubwa ya
mazingira haya inatawaliwa
na mimea ya kijani kama migomba mihogo na matunda ya aina mbalimbali .Kaa
ukijua kuwa chakula
cha wenyeji wa wilaya
hii ni ndizi.
Miinuko ,mabonde
na tambarare chache zinavutia
sana na ni
kwa sababu ufanya mwonekano wa sehemu
hii kuwa ya
kitalii Sambamba na hili utapata kuujua mlima wa
nchi jirani wa
mufumbiro ulioko nchini
Rwanda ambao pia nao
una maajabu yakee.
Hivi ni vivutio
vichache ambavyo vimesahaurika lakini bado tutaendelea kukufafahamisha zaidi
juu ya vivutio vigine zaidi
.Kazi kubwa ya
Mufumbiro tour and
safaris ni kuhakikisha tunaviweka wazi ili wanachi
tuvijue ,tuvitunze,vitupatie ajira na
tuijenge kyerwa yetu kwa pamoja
mufumbiro itakufahamisha jinsi
ya kujiunga katika mtandao wa
utalii wa dunia
nzima pia inalenga kukufahamisha
kujua umuhimu wa utalii .
Utalii ufanya
watu waishi katika
dunia moja ,kuimarisha
ushirikiano baina ya mtu
na mtu lakini pia utufanya
kufikia malengo yetu
baada ya kujua
ufahamu wa mambo yanayotuzunguka.Tunaitumia nafasi
kubwa kujadili uongozi
unavyoshindwa kutekeleza ahadi
zake hapohapo tukumbuke ni
siku gani tumejibidisha tukashindwa
kufanikiwa .Wanafunzi wengi wanasomea utalii nje
ya wilaya yetu wanafikiria
wafanye nini juu ya vivutio
hivi wewe pia upate kutafakari na kujijibu mwenyewe vivutio hivyo hapo tufanye
nini kufanikiwa na
vivutio hivi.Mufumbiro tour and
safaris inaamini itatoa
mwanga wa kutosha ili ushirikiane nayo
kuleta maendeleo katika Tanzania ya leo
na kesho.Kampuni hii inaamini
pia kuwa utalii ni wa kila
mtu awe mwenye pesa na hata
mtu wa aina yoyote
ile.Lakini haya yote kama
unaona kitendawili basi tembelea
matangazo yetu na
mitandao ili upate kujua
nini ufanye kampuni hii ni
nyota wa utalii
.Utapata kujua uchumi wetu
utakuaje kwa sababu utalii leo unaukuza uchumi
wan chi yetu kwa
asilimia kubwa sana au kwa
lugha rahisi uchumi
wa taifa unachangiwa
na asilimia kubwa kutokana
na kipato cha utalii .
No comments:
Post a Comment